Jumanne, 9 Julai 2013
Jumatatu, 8 Julai 2013
VODACOM YAZAWADIWA TUNZO YA KUWA MDHAMINI MKUU WA SABASABA
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda, akimkabidhi tuzo ya udhamini bora Meneja Malipo ya ziada wa Vodacom Tanzania, Liginiku Milinga, Kampuni hiyo iliibuka kidedea kwa kuwa mdhamini mkuu wa maonesho hayo na pia ilipata cheti kwa kushika nafasi ya pili katika sekta ya mawasiliano katika maonesho ya 37 ya kimataifa “Sabasaba” yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Pamoja nao katika picha ni Waziri wa viwanda na biashara, Mh. Abdallah Kigoda.
Meneja wa Malipo ya ziada wa Vodacom Tanzania, Liginiku Milinga akipozi katika picha baada ya kupokea tuzo ya mdhamini mkuu wa mawasiliano katika maonesho ya 37 ya kimataifa “Sabasaba” Tuzo hizo zilitolewa na Waziri Mkuu. Mhe. Mizengo Pinda.
WANAWAKE WAWILI WAMEKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA AFRIKA KUSINI WAKITOKEA TANZANI
Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na shirika la habari la Africa Kusini SABC siku ya Ijumaa (July 5), msemaji wa South African Revenue Services (SARS) Marika Muller amesema, wanawake hao waliowasili na ndege kutoka Tanzania, walikutwa na mabegi 6 makubwa yaliyojaa madawa (crystal meth) yenye thamani ya Rand 42.6 million ambayo ni sawa na zaidi ya billion 6 ya Tanzania.
Muller aliendelea kusema baada ya mizigo yao kuanza kukaguliwa ndipo timu ya maafisa uhamiaji iligundua kilo karibia 150 za madawa katika mizigo yao, kiasi ambacho ndio kikubwa kuwahi kukamatwa kama mzigo mmoja katika mpaka wowote wa Africa Kusini.
“When searching their luggage which was six large bags of black holdall bags, the customs team found just less than 150 kilos of crystal meth that is what we also call Tik in South Africa.
Those drugs are valued at R42.6 million which makes it the single largest seizure by the SARS customs team at any border in South Africa.” Alisema Muller.
Wanawake hao ambao hawakutajwa majina wala uraia wameshikiliwa na polisi nchini Afrika Kusini.
Jumapili, 7 Julai 2013
JANUARY MAKAMBA AWATAKA WANANCHI WAWALAUMU WABUNGE WAO KUHUSU KODI YA 1000 KWA KILA LAINI.....ADAI WIZARA YAKE ILIPINGA VIKALI
Haya ni majibu ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba akijibu maswali katika mtandao wa Twitter kuhusu kodi mpya ya TZS 1000 kwa mwezi kwa kila line ya simu.
- Amesema kwamba Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia iliipinga kodi hiyo.
- Amesema kwamba Hazina (Wizara ya Fedha) walikubaliana na maoni ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kuhusu kodi hiyo.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)