VODACOM YAZAWADIWA TUNZO YA KUWA MDHAMINI MKUU WA SABASABA
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda, akimkabidhi tuzo ya udhamini bora Meneja Malipo ya ziada wa Vodacom Tanzania, Liginiku Milinga, Kampuni hiyo iliibuka kidedea kwa kuwa mdhamini mkuu wa maonesho hayo na pia ilipata cheti kwa kushika nafasi ya pili katika sekta ya mawasiliano katika maonesho ya 37 ya kimataifa “Sabasaba” yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Pamoja nao katika picha ni Waziri wa viwanda na biashara, Mh. Abdallah Kigoda.
Meneja wa Malipo ya ziada wa Vodacom Tanzania, Liginiku Milinga akipozi katika picha baada ya kupokea tuzo ya mdhamini mkuu wa mawasiliano katika maonesho ya 37 ya kimataifa “Sabasaba” Tuzo hizo zilitolewa na Waziri Mkuu. Mhe. Mizengo Pinda.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni