WATU WATATU WAJERUHIWA KWA RISASI ZA MOTO BAADA YA KUKUTWA WAKICHEZA NGOMA ZA VIGODORO
Watu
watatu wakazi wa Mwananyamala Jijini Dar Es Salaam wamejeruhiwa katika
tukio lililohusisha risasi za moto linalodaiwa kufanywa na polisi baada
ya kukutwa wakikesha kwenye ngoma maarufu za Kigodoro, ambazo tayari
zimekwishapigwa marufuku na jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es
Salaam.Tukio hilo lilitokea majira ya saa kumi na nusu jioni katika eneo la shule ya msingi kisiwani ambapo mmoja
wa majeruhi hao tayari amekwisahruhusiwa kurudi nyumbani na mwingine
akiendelea na matibabu kwenye hospitali ya Mwananyamala.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni