
Inafikiriwa kuwa watu kadha waliuwawa katika
mashambulio yaliyofanywa na wale wanaoshukiwa kuwa wapiganaji Waislamu
kaskazini mwa Nigeria hapo jana.
Inasemekana kati ya waliouwawa ni askari wa usalama.
Baadae wanajeshi na ndege zilipelekwa katika eneo hilo na mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo, anasema maiti za wapiganaji kadha zimekutikana nje ya vijiji.
Mashambulio hayo yalifanywa karibu na Chibok ambako wapiganaji waliwateka wasichana wa shule zaidi ya 200 mwezi Aprili.
source: bbc
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni